Mchelea Mwana Kulia, Hulia Mwenyewe

Caroline Swai - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu na wanahitaji msaada au uangalizi kutoka kwa wazazi/walezi, jamaa, ndugu, majirani, marafiki na jamii kwa ujumla. Watoto wetu mara nyingi hutenda makosa bila kujua au kukusudia, hivyo inabidi wanapokosea tuwakanye na kuwapa adhabu ndogo ndogo ili kuwaonyesha kuwa wamekosea.

Endapo mtoto atakosea na ukaogopa kumkosoa, kumuonya au kumpa adhabu, mzazi/mlezi utakuwa unamlemaza, unamdekeza na kumfanya ajione kuwa ni mshindi na mjanja. Pia atajiona kuwa hakuna anayeweza kumweleza chochote, na kwamba yeye ni wa pekee. 

Hali hiyo ya kumchukulia mtoto kama anavyotaka, siyo nzuri kwani inaweza kumharibu na hatimaye akapotea kabisa. Hivyo wazazi/walezi na jamii yote kwa ujumla yatupasa tuwajibike, tuwakemee, tuwaonye na kuwapa adhabu ndogo ndogo pale inapobidi, pale wanapokosea. Kuwakanya watoto ni njia ambayo itawaokoa dhidi ya tabia hizo mbaya kabla ya kuzizoea au kukomaa kabisa.

Angalizo:

Tusipo wakanya watoto wetu sisi wenyewe, tutaishia kusema, "Mmnh! hawa watoto wana tabia mbaya sana”, huku tukiwa tumesahau kuwa sisi ndio tumesababisha wawe hivyo walivyo. Lilikuwa ni jukumu letu la kuwaongoza katika njia ipasayo tangu awali, tangu wangali wadogo. Msemo wa “Samaki mkunje angali mbichi ni sahihi kabisa kwa watoto pia. Wanajitaji kuaswa ama kuonywa wakiwa wadogo, tukichelewa kunakuwa hakuna matunda mazuri.

 Funzo: 

Wazazi na wadau wote tusikwepe kuwatunza na kuwaonya watoto pale wanapokosea bali tuwajibike ipasavyo. Hata kama siyo mtoto wako, timiza wajibu.

kama mwana jamii, kwa sababu mtoto wa mwenzio ni wako. Watu wengi lakini huwa hatuoni hivyo. Tabia ya kujali cha kwako ndio imetawala mioyo ya watu wengi.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Hakuna Tajiri Anayemjali Maskini, Na Hakuna Maskini Anayemhurumia Tajiri

Next
Next

Hakuna Siku Utakayomaliza Matatizo Yako Yote