Hakuna Siku Utakayomaliza Matatizo Yako Yote

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Matatizo yameumbwa kwa kila binadamu aishiye hapa duniani. Pamoja na kwamba tunajitahidi kuweka mikakati ili kutekeleza mipango yetu, ni mara chache sana tutaweza kutimiza malengo tunayokuwa tumejipangia. 

Mipango yetu ni kwa ajili ya kutuongoza ili tupate kujua kipi kimewezekana na kipi bado. Mara nyingi tegemeo lako haliendani na uhalisia wa utekelezaji. Lakini kinachotakiwa ni kuendelea mbele na mipango yako bila kukata tamaa. Kwa kile ambacho umebahatika kukifanya, yakupasa ushukuru huku ukiwa na imani kuwa hata lile lililobakia au kushindikana, litakuja kufanyika kwa wakati mwingine. 

Usiangalie mambo ya wengine au usijilinganishe na mtu mwingine. Songa mbele maana hakuna siku hata moja ambayo utaweza kumaliza matatizo yako yote. Kumbuka, mwisho wa tatizo moja, ni mwanzo wa tatizo jingine. Maisha ndivyo yalivyo. Yatupasa tujue hilo na tuzoee ili tuweze kujua namna ya kutafuta mbinu za kutatua changamoto tunazopambana nazo.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Mchelea Mwana Kulia, Hulia Mwenyewe

Next
Next

Mkopo Wasababisha Mama Akimbilie Mafichoni