Usikate Tamaa Kwa Kuwa Jua Limezama Wakati Nyota Na Mbalamwezi Hutoa Mwanga Pia

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Usemi huu unatumika pale tunapokuwa tumekata tamaa baada ya kushindwa kwenye mipango tuliyokuwa nayo. Ni kawaida ya watu wengi kukata tamaa pale tunapokuta mambo hayaendi vile tunavyotarajia ama tulivyokuwa tumepanga.

Wengi wetu, ama kila mtu, mathalani, anapofanya biashara, anategemea kila siku iwe ya neema kwake, anataka awe anapata kila siku. Ni rahisi kwa binadamu kusahau jinsi Mungu alivyotupangia. Pale unapokosa, pengine inakuwa ni mipango ya Mungu. Huwezi jua kilichosababisha ukose, kunaweza kukawa na sababu nyingi tu. 

Tusitarajie kuwa siku zote zitakuwa sawa. Ni kawaida mtu anapopatwa na hayo kulalamika na kunung’unika sana. Anaweza hata akawakatisha tamaa wengine. Lakini tunashindwa kujua kuwa mtoaji riziki ni Mungu na sote tunamtegemea yeye. 

Kama binadamu, tunatakiwa kuelewa kuwa ukikosa leo kesho utapata. Tunachotakiwa kufanya ni kushukuru kwa kile upatacho leo, ukijua kwamba ipo kesho ambayo inaweza ikawa ya baraka zaidi kwako. Hiyo sasa inategemea wewe unaamini nini na pia imani yako ni kubwa kiasi gani. 

Usemi huu una busara nyingi zilizojificha ndani yake. Inaonyesha shida unazopitia leo zinakufanya uone kuwa mbele yako kuna giza linalokuzuia usiende mbele. Lakini hapo hapo, pamoja na giza hilo, kuna nyota na mbalamwezi ambazo zinaweza kukuongoza tena ili kukutoa kwenye giza hilo na kuibadilisha hali unayopitia na hatimaye, ukaweza kusonga mbele.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Ni Vizuri Kujua Kila Kitu Lakini Siyo Vizuri Kusema Kila Kitu

Next
Next

Sio Sahihi Kila Mtu Kujua Changamoto Zako