Ni Vizuri Kujua Kila Kitu Lakini Siyo Vizuri Kusema Kila Kitu

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Kufahamu au kujua mambo ni utashi ambao Mungu amemjalia kila mwanadamu. Lakini katika kufahamu huko tunapaswa kuelewa mipaka ya ufahamu wetu na namna ya kukitumia hicho tunachofahamu.

Kuna watu ambao huwa tunasema hawana kifua. Watu hawa wakilipata jambo lolote huwa hawezi kukaa nalo moyoni. Watu wa namna hii huona kuwa ni lazima walipeleke jambo hilo kwa watu wengine. Hiyo ndio inakuwa furaha yao. Mara nyingi, hawafanyi hata upembuzi wa kuwawezesha kujua kama jambo hilo linafaa kupelekwa kwa watu ama laa. Watu wa aina hii ni wale wenye tabia ya uongo na uchonganishi. Wao hupenda kutangaza mambo ya watu. Watu hawa kwa kawaida, huwa hawajali kusema jambo la mtu, hata kama ni jambo la kuumiza.

Kama binadamu, tunatakiwa tuwe na vifua vya kutunza mambo ya watu. Inatupasa tuwe wasiri, tuheshimu mambo ya wengine. Hata kama mmekosana, si vizuri wala busara kuongea mambo yake na habari zake unazozijua. Kujua habari za mtu, siyo tiketi yako ya kuzitangaza kila mahali. Kumbuka kuwa ukubwa wako wa umri ni pamoja na kutunza siri za watu, na hata za wale uliokosana nao. Ukizingatia hayo, utaheshimika na kila mtu. Utakuwa dawa kwa wanaokuzunguka na siyo shubiri kwao. 

Kufarakana ni jambo la kawaida, linakubalika na huwa linapita. Kama binadamu tunaopita hapa duniani, hatuna sababu ya kuwekeana visasi kwa kutangaza mambo mabaya yaliyopita ya hasidi wako. Kukoseana ni kitu cha kawaida, kusameheana ni wajibu. Mnaweza kuwa mlikuwa marafiki wakubwa wa kuambizana siri zote. Ikaja wakati mkafarakana. Pamoja na kwamba ulikuwa unajua kila kitu, kibaya na kizuri cha swaiba wako, kwa vile sasa mmefarakana, hutakiwi kusema mambo yake kwa watu.

Huo sio ubinadamu hata kidogo. Tujifunze kuwa waungwana ili tuweze kuishi vizuri na wenzetu hapa duniani. Tupo hapa duniani kwa muda mfupi tu, yatupasa tuzingatie hilo.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Usimtendee Mwenzako Usiyopenda Kutendewa

Next
Next

Usikate Tamaa Kwa Kuwa Jua Limezama Wakati Nyota Na Mbalamwezi Hutoa Mwanga Pia