Kila Changamoto Ni Somo, Na Kila Mpango Ni Hatua

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Changamoto katika maisha ni lazima zimpate kila mtu anayeishi. Bila changamoto huwezi kusonga mbele ama kukamilisha malengo na mipango yako. Tukumbuke kuwa katika mipango tunayoitengeneza, ndio huwa mwanzo wa changamoto zake. Bila changamoto, huwezi kutekeleza yale uliyoyapanga. Hivyo basi, changamoto ni budi ziwepo.

Kuna wakati tunapopitia changamoto huwa tunapenda kulaumu watu na kuona kuwa wao ndio visababishi vya yale tunayopitia. Kwa kawaida, lawama hizo huwa haziangalii ukweli wa mambo. Huwa zinatolewa tu bila ya kuwa na uhakika kama wale tunaowadhania kweli wanahusika nayo. Hiyo si sahihi hata kidogo. Yatupasa kwanza tutafakari ili tuweze kuelewa cha kufanya. Pamoja na hayo, inatubidi utafute kila njia ili tuweze kutoka hapo tulipo. Hatutakiwi kukwama bali ni kusonga mbele. Huo ndio mwendo unaotakiwa na binadamu..  

Hatuna haja ya kuwakosoa watu kwa mabaya yao tunayoyafikiria, wakati hata hatuwezi kuwasifu kwa mema yao wanayotenda. Sote binadamu tuna mapungufu, tena makubwa tu. Hakuna mwanadamu ambaye ni mbaya asilimia mia moja. Kila mtu ana ubaya na uzuri wake, yatulazimu tutambue hilo. 

Usemi huu unatufundisha kwamba kila mtu ‘alijaliwa’ kuishi na sio ‘kujaribu’ kuishi. Wataalamu wengi wanatufundisha mengi tu kuhusu kukabiliana na changamoto zetu. Hii ni kutokana na ukweli kwamba, kila mtu anapitia changamoto za aina mbali mbali. Tofauti ni kwamba hizo changamoto zinazidiana uzito wake. Hali kadhalika, ni dhahiri kuwa kila mtu hupewa changamoto kwa kadiri ya uwezo wake wa kuzihimili.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Figa Moja Haliinjiki Chungu

Next
Next

Upendo Unaweza Kuwa Wa Kinafiki, Chuki Huwa Ni Halisi