Figa Moja Haliinjiki Chungu

Caroline Swai - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Figa ni chuma au jiwe ambalo hutengenezwa kwa ajili ya kushikilia chungu au sufuria wakati wa kupika jikoni. Kimsingi figa moja au mawili hayawezi kushikilia sufuria jikoni kwa ufanisi kwani sufuria haitakaa vizuri au kwa uimara jikoni. Ili sufuria ikae kwa uimara jikoni, ni lazima mafiga yawe matatu.

Mfano wa figa moja ni mtu mchoyo, anayejifanya anajua zaidi, anajiweza peke yake na anajitenga bila kutaka msaada au ushirikiano wa wenzake. Inaweza ikatokea kwamba endapo atashindwa kuendelea na shughuli zake, huweza rudi kwa wenzake kutafuta msaada, lakini huwa ni kwa aibu. Ikumbukwe kuwa, hakuna binadamu aliye kamilika. Binadamu tunahitajiana, huo ndio ukweli wa maisha.

Mfano mwingine wa mafiga matatu ni pale mtu anapokuwa na ushirikiano wa karibu na wenzake na hatimaye akawa na uwezo wa kukamilisha kazi zake vile inavyotakiwa na kwa mafanikio.

Hapa tunajifunza somo moja zuri sana, ambalo ni ushirikiano na watu katika mambo yoyote yawayo. Tunaposhirikiana na wenzetu tunapata fursa ya kupata uzoefu, uthubutu na ujasiri wa kutekeleza shughuli zetu za kila siku. Isitoshe, ushirikiano na watu wengine katika kazi yoyote husaidia kazi kufanyika haraka na kwa muda unaotakiwa na pia kwa ufanisi zaidi.

Tunaposhrikiana na wenzetu katika kazi na mambo mengine inakuwa kama vile mafiga matatu yanavyoshirikiana katika kukibeba chungu jikoni.

Misemo mingine inayofanana na msemo huu ni kama hii ifuarato:
“Kidole Kimoja Hakivunji Chawa”,
“Umoja ni Nguvu” na
“Utengano ni Udhaufu."

Misemo yote hii inatumika kwa lengo la kuonyesha umuhimu wa kuwa na ushirikiano katika jamii. Hakuna mtu ambaye ni kisiwa.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Ukiona Neno, Usiposema Neno, Hupatikani Na Neno

Next
Next

Kila Changamoto Ni Somo, Na Kila Mpango Ni Hatua