Asiyekuwa Na Hili, Ana Lile

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Usemi huu unatufundisha kuwa binadamu tunatakiwa kuheshimiana katika kila hali. Hakuna sababu ya binadamu mmoja kujiona kuwa ni bora zaidi kuliko mwingine. Mungu alipomuumba mtu na viumbe vyote, alivipatia karama, kila kiumbe tofauti na ya mwingine. Ndio maana unakuta kila mtu ana taaluma yake tofauti na ya mwingine.

Pamoja na kutofautiana huko, bado inatupasa tutegemeane. Kama vile vidole vilivyo havilingani, bado kila kimoja kina kazi ya kusaidiana na kingine kwa ufanisi zaidi. Na hivyo ndivyo hata sisi tunavyotakiwa kusaidiana/kushirikiana katika kila jambo tulitendalo.

Shirika la Tewwy limekutanisha akina mama waliostaafu. Kila mmoja wa akina mama hawa ana kitu au ufahamu ambao mwingine hana. Huu ni utajiri wa pekee. Hii ina maana kuwa tunapofanya kazi, yatupasa tuwe na imani kuwa kuna mambo mengi ya kujifunza kutoka kwa kila mmoja wetu. Hivyo inatulazimu kusaidiana ili tuenende vizuri na mambo tiliyojipangia, mambo ya unasihi. Ina maana kuwa kila mmoja wetu ana jambo analolijua ambalo mwingine halijui. Tunachotakiwa kufanya ni kuunganisha ujuzi na uzoefu wetu ili tuweze kupata mafanikio makubwa zaidi.

Kitu cha msingi ni kushirikiana kwa kupeana mawazo ili kuboresha yale tunayoyafanya. Ikumbukwe kuwa mtu mmoja hawezi kujua kila kitu, hata kama ni kiongozi. Ushirikishwaji katika maamuzi, hata kama wewe ni kiongozi na pengine unayafahamu mengi, ni muhimu katika upatikanaji wa matokeo chanya. Yatupasa tukumbuke na kuamini kuwa, asiyejua hili, ana lile. Endapo mawazo ya akina mama hawa wenye busara yatawekwa pamoja, tutaweza kupata mafanikio tunayoyategemea kutoka kwenye kazi hii ngumu iliyo mbele yetu.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Baba, Mama, Wote Tuwajibike

Next
Next

Aliyekula Vizuri Utamjua Wakati Wa Kunawa Mikono