Baba, Mama, Wote Tuwajibike

Simulizi
by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Kuwajibika ipasavyo ni jambo la lazima kwa binadamu kwani usipowajibika kuna mahali hapatakaa sawa, yaani panaweza pakaharibika. Baba kama kiongozi wa familia anatakiwa kutimiza wajibu wake wa ubaba vile inavyotakiwa. Anapaswa kuiongoza, kuitunza, kuilinda na kuihudumia familia yake ambayo aliianzisha. Hii inatuambia kuwa, kuitwa baba siyo kuwa mwanaume suruali bali ni kuwajibika kwa kila hali kama mzazi.
Vivyo hivyo, ukiwa mama au mwanamke unapaswa kutimiza wajibu wako kama mama wa familia. Ni lazima uhakikishe unaitunza familia yako kwa kuwapatia huduma wanazohitaji. Kwa maana nyingine, nyote wawili, msipofanya hivyo, yaani msipowajibika, mtabakia mnatupiana mpira kwa kulaumiana. Mama atamlaumu baba, hali kadhalika, na baba atamlaumu mama. Sababu kubwa ya kulaumiana ni kwamba, wote kama wazazi, hamkuwajibika ipasavyo tokea awali.
Hivyo wazazi wote tunapaswa kuwajibika kwa kutunza, kuhudumia na kuwa karibu na familia zetu ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea baadaye.
Msemo unaoendana na haya mazungumzo ni ule unaosema "Heri nusu shari kuliko shari kamili."Hii ina maana kuwa, ni bora kuchukua tahadhari mapema kuliko kusubiri janga litokee baadaye kwani kwa kufanya hivyo, utakuwa umechelewa.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection