Huwezi Kupanda Ngazi Ya Mafanikio Ukiwa Umeweka Mikono Mfukoni

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Ni jukumu la binadamu wote kuwajibika katika maisha yetu ya kila siku. Huwezi ukafanikiwa bila kutoka jasho. Kufanya kazi kwa bidii, ndio siri kubwa ya mafanikio ya mwanadamu.

Hakuna kitu kitakujia tu ukiwa umekaa. Kila siku tunalalamika kuwa hali ni ngumu, maisha ni magumu. Ugumu wa maisha umekuwa ndio wimbo wa kila siku, kwa walio wengi. Tukiangalia kwa undani, tunaona kuwa ni ile hali ya kutojishugulisha. Tabia hii ya kubweteka, ipo sana, hasa kwa vijana wetu.  

Asilimia kubwa ya vijana ni tegemezi. Wengi, eti wanasubiri ajira za serikali. Kujiongeza kwao ni neno lisilowezekana. Wao maadam wamesoma, wanaona hiyo ni silaha tosha. Vyeti vyao vinawasumbua, wanaona ndio suluhisho la maisha yao. Hata ukiwaambia ama kuwashauri kuwa wajishughulishe kwa namna moja ama nyingine, wao wanaona shida kweli kweli. 

Kwa kifupi, vijana hawa wanakuwa na ndoto za Alinacha, ndoto zisizokuwa na uhalisia wa maisha hata kidogo. Wako tayari kusubiri kwa kuweka mikono yao mfukoni. Ukweli ni kwamba, hawawezi kuona mafanikio kama hawatajishughulisha.  

Sisi kama wazazi/walezi/washauri, yatupasa tuendelee kuwasihi vijana wetu kuwa wajishughulishe na wawe tayari kufanya kazi za aina yoyote. Ikumbukwe kuwa, kazi ni kazi ili mradi mkono uende kinywani. Vijana wasichague kazi za kufanya. Shahada zao haziwezi kuwa chakula bali wakifanya kazi watapata fedha ambazo zitawasaidia kupata mahitaji yao ya muhimu, mahitaji ya kibinadamu.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Ukishindwa Hili Leo, Kesho Utashinda Lile

Next
Next

Kama Huwezi Kuwa Wa Msaada, Basi Usiwe Kizuizi