Hekima Ni Jambo La Msingi

Simulizi
by Victoria Nakajumo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Kile unachokiita baraka au ushindi kilianza kama tatizo. Mara nyingi, yule anayefanikiwa kutatua matatizo huonekana kama ana baraka au mshindi fulani hivi. Ni kawaida kwa kila mwanadamu kupata matatizo. Pale mtu anapopata matatizo, ni vema kutafuta mbinu za kupambana nayo. Wengi hujaribu kukimbia matatizo yanapotokea.
Ni vema ieleweke kuwa kukimbia matatizo ni kama kuyaahirisha tu. Matatizo yanaweza kukufuata popote utakapokuwa. Vile vile, yanaweza kujirudia yale yale uliyoyakimbia huko utakakokuwa umekimbilia. Na pale yatakapokukuta huko, unaweza kuwa na wakati mgumu zaidi. Unaweza kuogopa kukimbia tena, usije ukaonekana kuwa, wewe ndio ulikuwa ndio tatizo lenyewe.
Wapo wengi ambao walikimbia wenza wao na kwenda kwingine. Yalipowakuta huko, waliona kuwa walikotoka kulikuwa na unafuu zaidi. Walitamani kurudi lakini walishindwa kwa kuona haya. Kutokana na hali hiyo, walilazimika kuvumilia na hata kunyamaza kabisa.
Pamoja na kwamba wanaweza kuwa kwenye maumivu makali, wanakuwa hawana jinsi. Wanakosa mahali pengine pa kwenda. Hali kadhalika wanakuwa hawana hata mtu wa kumweleza yale yanayowasumbua. Baadaye wanakuja kutambua kuwa kumbe tatizo lilikuwa ni wao wenyewe.
Tunajifunza kuwa, katika maisha inatupasa kufanya maamuzi sahihi. Mambo ya kukurupuka, kamwe hayafai katika maisha yetu hapa duniani, mwisho wake huwa mbaya na wenye majuto tele.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection