Ziba Mwanya Usiruhusu Panya Kupita

Caroline Swai - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Mwanya ni nafasi yoyote ambayo mtu au kitu kinaweza kupita au kupenyeza bila kizuizi. Unaweza kuwa mwanya mkubwa au mwanya mdogo, alimradi hauzuii kilichokusudiwa kupenyeza. Hii ina maana kuwa, jambo lolote linapoanza kuharibika, huanza kidogo kidogo au taratibu sana na wakati mwingine bila hata kutambua.

Kwa mfano, ukuta wa nyumba unapoanza kupasuka, huanza kidogo kidogo. Endapo hutachukua tahadhari kuuziba mwanya huo mapema, ni dhahiri kuwa utaishia kujenga ukuta wote kutokana na uharibifu mkubwa utakaokuwa umejitokeza.Kwa hiyo tunashauriwa kuwa, mara unapoona jambo lako linaanza kuharibika, hasa katika hatua za mwanzo, anza kudhibiti hali hiyo mapema ili kuepuka hasara au madhara yanayoweza kujitokeza baadaye.

Usemi huu unatufundisha kuwa makini mara tuonapo uharibifu unaanza kujitokea hata kama utakuwa ni mdogo kwa kiasi gani. Tusidharau, tujifunze kuwahi kurekebisha jambo mara linapotokea, ni muhimu sana kwa ajili ya kuepusha hasara, madhara na mambo mengine yanayoweza kutokea kutokana na uharibifu huo.

Kimsingi, tuepuke kudharau ama kutozitilia maanani, changamoto ndogo ndogo, bali tuhakikishe tunazitatua mapema ili kuepusha shari. Msemo huu unaendana na ule usemao, "Usipoziba Ufa, Utajenga Ukuta." Sote tunajua kuwa kujenga ukuta ni gharama kubwa sana na ndio maana tunahimizwa kuchukua hatua mapema, mara tu tatizo linapotokea.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Mawazo Ya Watu Wenye Hekima Ni Kama Shamba

Next
Next

Mwongo Huwa Hasemi Yake