Tuchukue Tahadhari Stahiki, Dunia Inabadilika Kwa Kasi Mno

Simulizi
by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Ni ukweli usiopingika kuwa dunia inabadilika kwa kasi kubwa sana kila kukicha, mithili ya mtu aliyegeuza miguu juu, kichwa chini. Dunia ya leo siyo kama ile ya zamani. Dunia ya sasa imekuwa na mambo mengi ya aibu, maovu ya kutisha na ya kusikitisha kiasi kwamba ubinadamu au utu umetoweka. Imefika mahali hatuna huruma tena, tumekuwa kama wanyama. Mambo mengi mabaya yanaibuka kila siku na hata usalama wa binadamu upo mashakani.
Baadhi ya mifano inayoonyesha kuwa dunia inababadilika kwa kasi ni hii ifuatayo: vita kati ya nchi na nchi, wivu wa kimapenzi, mahusiano mabaya kati ya vijana na vijana, wazazi na wazazi, magomvi, roho ya kwa nini, kinyongo, usafirishaji na utumiaji wa dawa za kulevya, utumwa wa ngono, ushirikina na hata vifo vitokanavyo na kuuana. Mengine ni familia kuwatesa na kuwanyanyasa watoto wao wenyewe huku watoto wadogo wakilawitiwa na kubakwa hata na wazazi wao wenyewe> Watoto wamekuwa in wahanga wa maisha yao kwani hawawezi kijitetea. Hali inatisha kwani haingii kichwani unapomuona mzazi anamlawiti mtoto wake mwenyewe wa kumzaa. Dunia inakwenda wapi? Utu uko wapi? Tunatamani dunia isimame ii tusioweza kuendana na spidi yake hiyo. tuweze kuteremka.
Yote hayo yamebebwa ndani ya methali inayosema, "Dunia ni tambara bovu" huku amani furaha na upendo vikitoweka na ghasia zilkisheeni.
Simulizi hii inatukumbusha kuwa makini na matukio yanayotokea duniani na kututaka tuchukue tahadhari stahiki na madhubuti. Tukishindwa kufanya hivyo, tunaweza kuendelea kubakia kwenye ile dunia ambayo ni tambara bovu.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection