Mfungwa Hachagui Gereza

Margaret Kayombo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Margaret Kayombo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Huo msemo niliujumuisha na usemi ambao tumezoea kuuzungumza. Msemo huo ni ule wa: 'Sheria ni msumeno ambao unakata kote kote'. Nilishuhudia tukio hili nilipokuwa nasafiri toka Mwanza kuja Dar. Tulipofika Shinyanga tuliona abiria watatu wameingia kwenye basi tulilokuwemo. Mmoja wa abiria hao alikuwa amefungwa pingu.

Tulipowaona abiria wapya, bila kusita tulijua hao wengine wawili ni askari Magereza na yule mwingine alikuwa mhalifu. Walivyoingia ndani ya basi, walipewa viti vya kukaa. Walipoketi kwenye viti vyao, walimfungua pingu yule mfungwa. Walipofika Dodoma walimfunga tena ile pingu wakashuka naye.

Tukio hilo lilisababisha kuwepo gumzo kubwa ndani ya basi baada ya wale askari na mfungwa wao kuteremka kutoka kwenye basi. Kuna waliosema, "Masikini mfungwa huyo, hata anakopelekwa wala hajui". Wasemaji wengine nao walinena, "pengine hata ndugu zake hawajui kinachompata mwenzao, na wala hata safari hiyo hawaijui kabisa".

Palikuwa na mjadala mrefu ndani ya basi. Abiria wengine walisema, "Jamani yatupasa tujifunze haya tunayoyaona, ya polisi na mfungwa. Kama tuna mambo ya ajabu tunayoyafanya, inatulazimu tuyaache. Inauma kumuona mtu anasafirishwa na kwamba hata hajui anakwenda wapi. Hata mzigo ukisafirishwa huwa unaandikwa jina na namba ya simu ya mhusika mzigo unakokwenda".  

Kutokana na hayo niliyoshuhudia, huo msemo wa mfungwa hachagui gereza, ulinipa mawazo machache kuhusu maisha yetu. Ni muhimu sana kwa sisi wazazi pamoja na watoto wetu kujitahidi kuishi maisha ya kutii amri bila shuruti ili tuepukane na mateso na aibu inayotokana na uvunjaji wa sheria, taratibu na kanuni za nchi. Sote tunajua kuwa sheria haina umri, sote inatubidi tuishi maisha yenye maadili, maisha ambayo hayawezi kutupelekea kwenye mikono ya sheria na mwisho wake kupata mateso ambayo yatatukosesha amani ndani ya familia. Mateso haya yanaweza kutusababishia matatizo mengi yakiwa ni pamoja na afya ya akili. Mungu atusaidie.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Tuache Ukatili Kwa Wanyama, Malipo Ni Hapa Hapa Duniani

Next
Next

Tuchukue Tahadhari Stahiki, Dunia Inabadilika Kwa Kasi Mno