Tuache Ukatili Kwa Wanyama, Malipo Ni Hapa Hapa Duniani

Simulizi
by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Palikuwa na kijana mmoja ambaye alirithi mifugo kutoka kwa baba yake. Hivyo alikuwa mfugaji na mchungaji. Miongoni mwa mifugo aliyorithi, walikuwepo punda, ng'ombe, mbuzi, kondoo, mbwa na kadhalika. Akiwa machungani alikuwa na tabia mbaya ya kuitesa baadhi ya mifugo yake. Moja kati ya wanyama aliyekuwa anateswa sana ni punda ambaye alikuwa anamsadia kubeba mizigo.
Siku moja alimziba punda mdomo, akamfunga kamba shingoni kisha akamfungia kwenye mti. Alianza kumpiga kwa kutumia fimbo, makofi na mateke. Mateso na maumivu hayo yalipozidi na kuwa makali sana, punda alipandisha hasira. Alimgeuzia kibao mwanadamu huyo katili. Naye alianza kumrushia mateke ya nguvu. Hatimaye alimng’ata kwenye mguu, akawa anazunguka naye hadi mguu ukavunjika.
Kijana alipata maumivu makali sana. Alijuta kutenda ukatili huo kwa mifugo yake. Aliahidi kutorudia tena matendo hayo maovu.
Simulizi hii inaendana na methali zifuatazo; “Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu uchungu", "Mtenda, hutendwa", na "Mwosha, huoshwa."
Hapo tunajifunza kutokuwa wakatili kwa mifugo yetu. Mifugo nayo ina miili ambayo huumia pale inapofanyiwa ukatili.
Isitoshe, yatupasa tutambue kuwa wanyama wana haki zao za msingi zinazowalinda. Haki hizo ni pamoja na kulishwa, kutunzwa vizuri, kupatiwa maji ya kutosha na kutibiwa pindi wakiugua. Hali kadhalika, wanahitaji kuwekwa kwenye mabanda mazuri na safi ya kulala. Kwa ujumla, wanahitaji mazingira safi.
Hali kadhalika, ikumbukwe kuwa mifugo tunayofuga ni kwa matumizi na faida yetu sisi binadamu. Hivyo, inatulazimu kuacha ukatili kwa mifugo yetu.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection