Cha Mtu Mavi

Simulizi
by Margaret Kayombo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Tunaishi duniani kwa viwango tofauti vya maisha. Kuna baadhi ya watu wanavyo vitu vya kupitiliza, hadi inakuwa kama kufuru. Wengine wanavyo vya wastani, na wengine wanavyo kidogo au hawana kabisa. Kutokana na hali hiyo wanadamu tunaishi kwa kutoridhika na hivyo tulivyo navyo.
Kutokana na hizi hali mbalimbali, binadamu wengine huanza kujawa na hisia za wivu au chuki kwenye mioyo yao na hata kuwapelekea kutoa maamuzi magumu na mabaya kwa jirani, rafiki na hata kwa ndugu zao. Maamuzi magumu na mabaya yanaweza kumshawishi mtu kujiuliza, "kwa nini yeye na siyo mimi"? Hali hiyo inamshawishi mtu kuingiwa na roho ya uharibifu mpaka inampelekea kuiba mali za wengine au kufanya nambo mengine mabaya, ili mradi mwenye chake aumie.
Lakini na mhusika pia, ambaye ndiye mtenda maovu, pia huishia kupata kesi na kuishia kufungwa. Hata familia yake hudhalilika sana kutokana na uovu wake. Hali kadhalika, tunashuhudia mifarakano mingi kutoka kwa marafiki. jamaa na hata kwenye koo zetu. Amani na upendo baina ya binadamu hutoweka kutokana tu na wivu wa mtu anapoona mwenziye ana hiki na kile na yeye hana chochote. Dunia ni ya ajabu, imejaa wivu, husuda na mambo mengi mabaya yanayotendwa na binadamu.
Usemi huo wa 'Cha mtu mavi', unatufundisha kuwa turidhike na tulicho nacho. Endapo na wewe unataka kuwa navyo vingi kama vya yule, basi yakupasa ufanye kazi kwa bidii ili upate mafanikio. Kufanya uharibifu siyo njia sahihi ya wewe kufanikiwa. Vilevile yakupasa ujue kwamba cha fulani siyo chako. Endapo utakitamani, ni bora ukione kinanuka kama mavi. Kwa kufanya hivyo, ile hali ya kufanya maovu halafu upate kesi au uishie jela itakuepuka na hivyo utakuwa na maisha ya amani ndani ya moyo wako na mambo mengine yataendelea vizuri. Utaishi bila misukosuko kutokana na kutamani vya watu na kufanya uovu.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection