Barua Ya Moyo Husomwa Kwenye Paji La Uso

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Moyo ni kitu kidogo sana katika mwili wa mwanadamu. Moyo huwa hauonekani kwa jicho la kawaida, lakini moyo ndio uhai wa mtu ulipo. 

Moyo huwa unaongea pasipo kutamka neno. Moyo ukisimama hapo ndipo hata uhai wa mtu unakuwa umekoma. Moyo huua kwa fikira na kwa mawazo. Maamuzi ya moyo huwa hayana mpinzani. 

Mambo mengi yanayotokea katika maisha ya mwanadamu, moyo ndio chimbuko la kila jambo. Mara zote usipouzuia moyo, unaweza ukajikuta unafanya maamuzi ya kujilaumu.

Moyo unaongea na kukuelekeza nini ufanye. Unaweza kumugundua mtu kama kuna jambo analifikiria pale utakapo angalia kwenye paji lake la uso. Mtu huyo anaweza kuwa anawaza mambo chanya au hasi. 

Endapo utamshitua mtu huyo na ukaona anashtuka na kuguna, basi elewa kabisa kuwa hapo alikuwa mbali sana na ulimwengu huu. Mara nyingi hilo analofikiria linakuwa halina majibu. Na kama kutakuwa na majibu, basi majibu hayo yatakuwa hasi. Moyo unaua na kuhuisha. Moyo ndio kila kitu, moyo ndio uhai wenyewe.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Usimtekenye Aliyekubeba, Atakudondosha

Next
Next

Cha Mtu Mavi