Usimtekenye Aliyekubeba, Atakudondosha

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Maisha yetu ni ya kutegemeana kwa kiwango kikubwa sana. Hakuna mtu atakayesema hapa alipo amefika kwa juhudi zake mwenyewe. Lazima kuna mahali alifika akakwama, na mtu mwingine akamkwamua na hatimaye akatoka.  

Mara nyingi, mtu anapata kazi kwa kusaidiwa na mtu mwingine. Lakini inafikia mahali mtu akishazoea kazi anaanza kujenga tabia ya kusahau. Hamkumbuki tena aliyemsaidia na kumfikisha hapo alipo. 

Kuna dada mmoja aliajiriwa na kampuni moja binafsi kwa msaada wa mtu. Yule dada baada ya kuzoea akawa anatembea na meneja wake. Cha kushangaza ni kuwa yule aliyemsaidia kupata kazi ni mke wa yule meneja wake. Binadamu ni kiumbe wa ajabu, hakawii kusahau. 

Baada ya muda mrefu wa kuwa na yule baba alifikia hatua ya kuanza kuwadharau na kuwanyanyasa wenzake pale kazini. Wenzake waliona isiwe taabu. Walichukua hatua ya kumueleza mhusika yaani mwenye mali yake, ambaye ni mke wake wa yule meneja. Walimweleza kila kitu.

Kilichotokea mke wa meneja aliamuru huyo dada afukuzwe kazi mara moja bila malipo yoyote. Maskini dada wa watu, ilibidi arudi zake mtaani kuhangaika. Usicheze na ’mali’ za watu, eh bwana. 

Sambamba na usemi huu ni ule usemao ukitaka kula na kipofu usimshike mkono. Binti alisahau kuwa pale alipelekwa na mtu, na siyo mtu tu bali ni mke wa meneja ambaye dada huyo aliamua iwe mali yake. Alikosea sana kuamua kumbeba mume wa watu bila kukukmbuka fadhila alizofanyiwa na huyo dada mwenye mume. Mungu hutoa malipo hapa hapa duniani. 

Ona sasa yaliyompata. Kwa kukosa heshima na fadhila kwa yule aliyemtafutia kazi, amerudi mtaani na kuendelea na mihangaiko yake. Maisha ni ya ajabu, hayana formula. Ukitenda mabaya kwa wenzio, malipo yake huwa ni hapa hapa duniani. 

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Yatima Hadeki

Next
Next

Barua Ya Moyo Husomwa Kwenye Paji La Uso