Yatima Hadeki

Simulizi
by Margaret Kayombo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Neno yatima au ukiambiwa yule ni yatima kila mtu ataelewa. Yatima ni mtoto ambaye, aidha kafiwa na mzazi mmoja au kafiwa na wazazi wake wote wawili.
Katika maisha yetu ya kila siku tunakumbana na yatima wengi. Hali kadhalika, tunashuhudia mambo mengi wanayopitia. Unaweza kukuta yatima wengine wanaishi vizuri lakini walio wengi wana changamoto za kusikitisha. Kuna kitu huwa kinaibuka kwa wengi wakishapitia hali hii ya uyatima. Mara nyingi wanakuwa na hali ya kutokujiamini na hivyo huanza kutegemea misaada kutoka kwa ndugu. Ikifikia hatua hiyo, ndipo tatizo huwa linaanza .
Kuna mengi yanatokea katika mazingira haya. Huwepo ndugu ambao huonyesha kwamba wanachukua majukumu ya mzazi wao au wazazi wao. Hutokea kwamba majukumu wanayobeba huwa siyo sahihi. Hutokea uchu wa kutaka kudhulumu mali walizoachiwa na mzazi au wazazi. Mara nyingi, watoto hubaki wakinyanyasika na kukosa kabisa haki zao. Watoto wanakuwa hawawezi kuongea au kuuliza chochote kile kinacholetwa mbele ya macho yao. Hawawezi kudadisi kwa nini inakuwa hivyo. Pale inapotokea wanaletewa kitu, wawe wanakipenda ama hawakipendi, watajijua wenyewe.
Wakati mwingine watoto hutawanywa kwa lengo la kuwatenganisha na kupelekwa kule na huko, ili mradi tu wasiwe pamoja. Yote hiyo hufanywa ili tu mali za marehemu wazitumie wanavyopenda wao.
Ukatili mkubwa wanaofanyiwa yatima, ni jambo ambalo linadhohofisha sana ustawi wa watoto kwenye jamii zetu.
Tukiutafakari msemo huo hatuna budi kuliomba taifa liwaangalie yatima kwa jicho la pekee ili nao wawe na uhuru na haki ya kumiliki mali walizoachiwa na wazazi wao. Serikali iweke sheria za kuwabana ndugu ambao wanajiita ni wasimamizi wa mirathi ili wanapofikia hatua ya kugawa hizo mali wazipeleke mahakamani ili haki iweze kutendeka.
Maoni yangu mengine ni kwamba yatupasa ndugu tuonyeshe upendo kwa yatima na kuwapa msaada pale unapohitajika maana hatujui kesho yetu. Hali hii itawapelekea yatima kuwa na amani na kuishi kwa furaha kama wanadamu wengine. Yatupasa tuwekeze kwa yatima ili na sisi watoto wetu watakapokuja kuwa yatima, waweze kupata msaada kutoka kwa watu wengine. Maisha ni mzunguko, na uyatima hauchagui wala haubagui. nyumba wala familia.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection