Mpatie Mtu Ujira Wake Kwa Wakati Anaostahili

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Kuna aina nyingi za ajira hapa duniani. Usemi huu unawalenga wale tunaowaajiri hasa kwenye kazi za nyumbani (house girls). Kuna tabia mbaya ya baadhi ya waajiri kwenye sekta hii kutokuwajali na kuwathamini wafanya kazi wa sekta hii.

Kuna mama mmoja alikuwa na dada wa kazi ambaye alikuwa amekaa naye kwa zaidi ya miezi sita bila kumlipa kile walichokuwa wamekubaliana. Kila wakati msichana akimuambia kuhusu malipo yake, yule mama humtukana na kumsimanga vibaya. Aliweza kudiriki hata kumwambia kuwa hela zake za mshahara, zinanunua chakula anachokula.  

Kilichokuja kutokea siku moja, binti aliamua kuondoka na vitu vya thamani mle ndani. Aliweza kubeba mpaka nguo za mama na za baba. Kibaya zaidi, alimuachia mtoto wake wa miaka mitano pale nyumbani na geti likiwa wazi.  

Mama aliporudi jioni alimkuta mtoto kachoka na kulia na alikuwa hajala kitu chochote. Kila akimuuliza mtoto alikuwa hawezi kusema. 

Roho mbaya ya mama, hayo yalikuwa ndio malipo yake. Hakuweza kumfuatilia maana alikuwa hajui alikuwa anatokea wapi. Wengi wa wasichana wa kazi tunawaokota hapa hapa mjini. Natumia neno ‘kuokota’ kwa sababu katika hali ya kawaida, palipo na upendo, ni lazima utapenda kufuatilia na kujua atokako. Kumbuka, yeye ni binadamu, likitokea la kutokea sijui utafanya nini?  

Ni tabia ya kiungu kumlipa yule anayekutumikia kwa wakati. Ndivyo ubinadamu unavyotakiwa kuwa. Isitoshe, huyo mfanya kazi wako amebeba maisha yenu wote humo ndani. Ana uwezo wa kufanya chochote kibaya anachotaka kwenu. 

Yatupasa tuheshimu kazi wanazofanya watumishi wa ndani. Ni vizuri tukawafanya kama sehemu ya familia zetu. Tunawahitaji sana, na kazi zao ni za msingi sana katika maisha ya mwanamke aliyeajiriwa. Hebu tubadilike kama tuna tabia mbaya za kunyanyasa wasichana wa kazi za ndani. Nao ni binadamu, wanahitaji upendo kama watoto wako.  

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Usitumie Usomi Wako Kuwanyanyasa Na Kuwatambia Wenzako

Next
Next

Yatima Hadeki