Usitumie Usomi Wako Kuwanyanyasa Na Kuwatambia Wenzako

Simulizi
by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Wako watu wanaojiona, wanaojitapa na kutamba kuwa wana akili sana. Hujiona wamesoma na wameelimika zaidi ya wengine. Watu hawa huchukua fursa hiyo ya kuelimika kama fimbo ya kuwachapia wenzao. Huwanyanyasa wenzao kwani huwaona kuwa ni wajinga na pia hawana elimu. Hali kadhalika, huwadharau, kiasi kwamba hata kuongea nao inakuwa ni shida, kisa, eti hawajasoma.
Kujitamba na kujiona kuwa wewe umeelimika kuliko wengine ni kukosa hekima. Walioelimika, hawahitaji kujionyesha, kuringa, wala kujisifia sana kwani matendo na tabia njema, kauli nzuri, utulivu, hekima, busara, heshima na ukarimu ndivyo vitu vinavyomtambulisha mtu kuwa kuwa huyo ameelimika ipasavyo.
Hapa tunakumbushwa kwamba kuelimika kwa mtu kunadhihirishwa na mahusiano mazuri na matendo mema katika jamii yake, jamii inayomzunguka.Hivyo, tunaaswa kuwa, tusiitumie elimu yetu kwa hasara, bali tuitumie kwa faida katika jamii zetu.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection