Ujana ni Dhahabu

Caroline Swai - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Katika maisha tunaweza kusema kuwa, "umri wa ujana" ni kipindi cha dhahabu ambacho tunatengeneza marafiki wengi na kupoteza wengi pia. Katika kipindi hiki, uamuzi wa kuyaharibu au kuyatengeneza maisha yako ili yawe mazuri baadaye unao wewe mwenyewe. Kwa hiyo inakupasa kukumbuka kuwa kipindi hiki kikishapita hakijirudii tena. Hivyo kitumie vizuri uwezavyo.

Wakati mwingine matendo ya kukuharibia maisha ya baadaye huonekaana mazuri na ya maana sana katika ujana, ambapo yale matendo ya kukufanya uishi vizuri baadaye huonekana siyo mazuri, sahihi na wala hayafai. Yatupasa tufanye maamuzi ya nini cha kufuata. 

Katika kipindi hiki tunafanya makosa mengi na kujirekebisha pia. Tunakurupuka, tunaanguka, tunaumizwa, tunashindwa, tunajifunza, tunagundua, tunachanganyikiwa na wakati mwingine tunajipoteza wenyewe. Pengine kipindi hiki huenda ndiyo miaka ya neema katika maisha yako, hivyo unapaswa kutofautisha kati ya kuyafurahia au kuyaharibu.

Simulizi hii inatukumbusha kuwa, kipindi cha ujana ni mali, pia tunakiita “Ujana ni dhahabu”. Yatupasa tuutumie muda wetu wa ujana vizuri na kwa uangalifu na uadilifu. Katika kipindi hicho cha mapito makubwa na mazito, kamwe hatutakiwi kukata tamaa. Ni kuanguka na kusimama tu, hadi kieleweke.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Jifunze Kujishusha Machoni Pa Watu Wengine

Next
Next

Usitoe Maamuzi Wakati Una Hasira