Jifunze Kujishusha Machoni Pa Watu Wengine

Simulizi
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Baadhi ya watu wana ile tabia ya kuona kwamba wao ndio pekee wa kuweza kutoa maamuzi ya aina yoyote wakiwa kwenye kundi la watu. Tabia ya watu hawa ni ya kujiona na kujisikia kuwa wao ni bora kuliko watu wengine. Watu hawa hufikia hatua ya kuchukia pale wanapotoa jambo/ushauri mbele za watu na halafu usikubaliwe. Huwa hawaelewi kabisa kwa nini yale wanayosema yasikubaliwe na watu.
Tabia ya namna hii sio nzuri hata kidogo. Ni tabia ya kibinafsi ambayo ni lazima ipigwe vita. Ni vema kwa mwanadamu kuwa na moyo wa kujishusha. Si vema kabisa kujikweza. Hatupaswi kupambana na mtu hata kama tuna uwezo kiasi gani. Kamwe hatutakiwi kujionyesha kuwa sisi ni waamuzi wa kila jambo kwenye jamii yoyote. Yatupasa tuwasikilize watu wengine ili tuone wanasema nini ama wana mawazo gani kuhusu jambo hilo. Hatutakiwi kujisifu bali yatupasa tuache watu wengine ndio waone uwezo wako. Wewe jiachie ili uwe daraja kwa wengine.
Maandiko yanasema aliye juu mngoje chini. Usemi huu una maana kubwa katika maisha ya mwanadamu. Maisha ya mwanadamu ni kupanda na kushuka. Ukiishi ukijua namna ya kujishusha, utaratibu huo utakuwezesha kuwa na watu wengi wema watakaokuzunguka. Tujifunze kujishusha machoni pa watu. Huu ni uungwana.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection