Hakuna Mtu Duniani Anayeweza Kuziba Pengo La Mtu Mwingine

Simulizi
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Duniani kila mtu alikuja kwa wakati na majira yake. Hata mapacha waliigia duniani kwa muda tofauti. Kila mtu amekuja duniani kwa kusudi lililopangwa na Muumba wake. Katika hali hiyo hiyo basi, kila mtu ataondoka kwa wakati wake. Haijalishi kama mlizaliwa mapacha. Hii ina maana kuwa mmoja akiondoka, linabaki pengo lisilozibika.
Usemi huu unatufundisha kutoangalia anachofanya mtu mwingine. Ikumbukwe kuwa kila mtu ana kitu kilichopandwa ndani yake ambacho mwingine hanacho. Tuondoe roho ya kwa nini, bali tuwe na upendo na turidhike na kile tulicho nacho.
Hata makazini tunaona mtu anayefanya kazi vizuri huwa anapata changamoto sana. Mara nyingi huwa anasakamwa sana na wenzie na kunenewa maneno mabaya. Yote hayo hufanywa dhidi yake ili tu kumtoa kwenye utendaji wake mzuri wa kazi zake. Pengine hata kazi zile azifanyazo, wao hawana uwezo nazo. Hizo huwa ni husuda tu za binadamu, kwani binadamu ndivyo walivyo. Binadamu huwa hakosi cha kusema.
Ni dhahiri kuwa wanashindwa kuelewa kuwa hakuna mtu duniani awezaye kuziba pengo la mtu mwingine. Kila mtu ana nafasi yake katika kila jambo. Yatupasa kuacha ushindani usiokuwa na tija. Tunapaswa kuheshimu nafasi ya kila mtu katika maisha yetu.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection