Usitoe Maamuzi Wakati Una Hasira

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Hasira ni ile hali ya kuhamaki kwa jambo ambalo umesikia au umefanyiwa na mtu bila kukubaliana ama kuridhika nalo. Inawezekana likawa ni jambo la kusingiziwa au la. Hasira inaweza kukupelekea kuamua chochote kibaya, ukafikia hata hatua ya kuua. Mara nyingi,?hasira inaishia kwenye kujuta kwa lile ulilolifanya kwa kukusudia ama kutokusudia. Sambamba na usemi huu ni ule wa Majuto ni Mjukuu. Tunaaswa kutokuamua jambo lolote wakati tuna hasira. 

Kuna jambo limetokea hivi karibuni maeneo ya Charambe. Jambo hili linawahusu watoto wawili, mmoja wa kike mwenye umri wa miaka 9, na mwingine wa kiume, mwenye umri wa miaka 12. Watoto hao walikuwa wanagombania rimoti ya televisheni. Ni kawaida ya watoto kugombea rimoti, hii si ajabu. Yule mtoto wa kiume alimshinda mwenzie, ambaye ni mdogo wake wa kike kwa kuchukua rimoti. 

Cha ajabu, mama yao mzazi alianza kumpiga mwanae mdogo kwa sababu tu ya kugombania rimoti na kaka yake. Mila na desturi zetu zilizo nyingi, zinaonyesha kuwa na upendeleo kwa watoto wa kiume, eti wao ndio wenye haki ya kila kitu. Maskini yule binti baada ya kipigo alienda chumbani kwake akiwa na uchungu wa kipigo. 

Kilichotokea baada ya dakika chache mama alimfuata binti chumbani kwake ili aende kula chakula. Kwa taharuki na mshangao mkubwa alimkuta binti yake akiwa amefariki pale kitandani. Inasemekana alikuwa vidonge vingi vya kuondoa uhai wake. 

Wengi wanahisi kuwa mtoto aliamua kujitoa uhai wake kutokana na hasira ya kucharazwa viboko baada ya kugombania rimoti na kaka yake. Hii inaonyesha kuwa binti hana haki ya kubishana na kakake, kwa sababu, kwanza kakake alikuwa ni mkubwa kiumri. Pili, kufuatana na mila, mwanaume yuko juu ya mwanamke. Binti aliona kuwa amenyanyaswa sana na mamake na ndio ikawa sababu kwake ya kuondoa uhai wake. 

Kwa upande wa mama, tunaweza kusema kuwa alichotenda,ni matokeo ya hasira. Mpaka leo yule mama yuko polisi rumande. Maskini, hakuweza hata kumzika mwanae. Sheria ilichukua mkondo wake ilipogundulika kuwa kujiua kwa binti yule kulitokana na adhabu ya kipigo alichopewa na mamake. Hatujui mtoto alipigwa kiasi gani hadi kumsababisha kuchukua uamuzi wa kujiua.  

Mama amebaki na majuto, mtoto amempoteza na yeye yuko rumande akisubiri hukumu. Wahenga walinena, hasira hasara. Yatupasa tujitahidi kutoamua jambo tukiwa na hasira. Kitakachofuata, ni majuto matupu. Hebu tuangalie yaliyompata mwenzetu. Ni hatari tupu. 🙆🏽‍♂️

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Ujana ni Dhahabu

Next
Next

Heri Nitakula na Nani Kuliko Nitakula Nini