Heri Nitakula na Nani Kuliko Nitakula Nini

Grace Mshanga - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Maisha tuishio yapo katika matabaka tofauti. Wapo watu wenye uwezo sana, wapo wale wenye uwezo wa kati na wale wenye uwezo wa chini. Ni muhimu kujua kuwa maisha yetu sisi binadamu yanatofautiana.

Usemi huu unatukumbusha umuhimu wa kuwasaidia watu ambao wana uhitaji. Hii ni kutokana na tofauti zetu kiuchumi ambazo zinatufanya tuwe kwenye matabaka tofauti. Si ubinadamu hata kidogo unapomuona mwenzio anateseka ukamuacha bila msaada. Binadamu wengine ni wa ajabu. Huwa wako radhi hata kuwatupia mbwa chakula kuliko kuwasaidia binadamu wenzao wenye shida. Hao binadamu ambao hawana kitu ni viumbe wa mungu sawasawa na wewe. 

Lakini hapo hapo pia tunajifunza umuhimu wa kujituma na kufanya kazi kwa bidii ili kuondokana na utegemezi. Ukiwa mhangaikaji na Mungu akakujalia, utaweza kuepuka adha ya kunyanyapaliwa pale unapokuwa tegemezi. Pamoja na yote, binadamu yatupasa kusaidiana bila kudharauliana. Shida humpata kila mtu hapa duniani, maisha ndivyo yalivyo.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Usitoe Maamuzi Wakati Una Hasira

Next
Next

Ukipanda Cheo Usisahau Familia Yako