Ukipanda Cheo Usisahau Familia Yako

Simulizi
by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Cheo ni aina mojawapo ya usitawi au baraka azipatazo mwanadamu katika mazingira yake ya kazi. Hata mfanya biashara anapokuwa amekua kibiashara, nako pia ni kama kupanda cheo.
Mara nyingi watu wengi wakifikia hapo huwa wanasahau walikotoka na wanafikia hatua ya kuwanyanyasa hata wenzii wao. Wengi husahau kuwa cheo ni dhamana na hivyo hakuna sababu ya kukiringia.
Tunakumbushwa kuwa tupandapo katika maisha ama tunapopata fursa ya kuwa na kipato zaidi tusiwasahau ndugu zetu. Unapofanikiwa iwe ni kwa faida ya familia yako pia. Pengine mafanikio yako yamepatikana kutokana na maombi na uvumilivu wa familia yako.
Palitokea mama mmoja ambaye alikuwa mke wa Afisa mkubwa sana jeshini. Mume wake alikuwa na cheo cha Brigedia. Maisha ya mama huyu yalimwendea vizuri sana na hivyo alijiona kuwa ameukata na kuwa ‘matawi ya juu.’ Kutokana na hali hiyo ya utajiri, alikuwa anawadharau sana ndugu zake. Hakuwa na muda nao kabisa. Aliona kuwa hao ndugu zake walikuwa siyo wa hadhi yake.
Kama ilivyo ada, wakati ulipofika, mume alistaafu na hivyo kutokuwa kazini tena. Hali hiyo ya kustaafu ilianza kuleta mabadiliko katika utaratibu wa kimaisha. Maisha yalibadilika sana. Hali hiyo ilimsononesha sana mama huyu hadi akafikia hatua ya kupata ugonjwa wa kiharusi. Kutokana na kutokuwathamini ndugu zake wakati alipokuwa nazo, hakutokea ndugu yeyote wa kumtunza. Hivyo alipoteza maisha.
Simulizi hii inatufundisha kuwa tupatapo nafasi nzuri katika maisha, nafasi ya kifedha, yatupasa tuwajali wenzetu. Pia yatupasa tukumbuke kuwa maisha ni kupanda na kushuka. Hali kadhalika, maisha yana utaratibu ambao tunaweza kusema ni mzuri, utaratibu wa leo kwako, kesho kwa mwenzio. Maisha ni mzunguko, huwezi kuwa unapata kila siku ama unakosa kila siku. Kupata kunafanyika kwa zamu. Mtoaji ni huyo huyo mmoja na hana upendeleo wa aina yoyote. Hivyo ukipata, tulizana, usiwadharau wasio kuwa nacho.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection