Kinga ni Bora Kuliko Tiba

Grace Mshanga - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Kinga ni kudhibiti tukio au jambo kabla halijaleta madhara. Tukio linaweza kuwa ni ugonjwa au mambo mengine yawayo.

Simulizi hii inatufudisha kuchukua hatua ya kudhibiti tukio kabla halijaleta madhara. Hebu tuchukue mfano huu.  Watu wazima pamoja hata watoto wanatakiwa kumeza dawa za minyoo kila baada ya miezi mitatu. Lakini wengi wetu hatufanyi hivyo, tunaishia kulalama tu zaidi ya kuchukua hatua. Kwa kufanya hivyo, tunakuwa tunakaribisha magonjwa yasiojulikana. 

Palitokea mama mmoja ambaye alizembea kumpatia mtoto wake dawa za minyoo. Alijikuta yuko hospitalì, mtoto akiwa hoi bin taabani. Madaktari walijitahidi kumsaidia mtoto ili kuokoa maisha yake. Lakini ilishindikana. Ilibidi ufanyike upasuaji. 

Jambo hili lilimtesa sana mama kwani alijikuta amebaki kuuguza kidonda. Angefuata taratibu za kumpatia mtoto dawa wakati unaotakiwa, tabu hizo zisingemkuta. 

Pia kulikuwa na mama mwingine ambaye alikuwa amekaa na mumewe kwa miaka mitano bila ya kupata mtoto. Alienda hospitali kwa ushauri. Madaktari walimfanyia matibabu na kumpa masharti ya kutokunywa pombe wala kuvuta sigara. 

Mungu bariki, mama alipata ujauzito. 

Kutokana na mazoea ya kunywa pombe na kuvuta sigara, ilimuwia vigumu kuacha tabia hizo, hivyo aliendelea. Maskini mama huyu ambaye hakutaka kusikia ushauri wa wataalamu, yalikuja kumpata makubwa. Kwa bahati mbaya, alikuja kuzaa mtoto mfu. Kwa hakika kwa mama huyu usemi wa ‘Asiyesikia la Mkuu Huvunjika Guu ulikuja kumhusu. Laiti angelitii maagizo na masharti ya madaktari wake, hayo yasingemkuta asilani. 

Hivyo tunajifunza umuhimu wa kuzingatia ushauri tunaopatiwa na wataalamu mbalimbali kwa faida ya maisha yetu.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Ukipanda Cheo Usisahau Familia Yako

Next
Next

Tunza Siri za Kazi Zako kwa Mafanikio Yako