Tunza Siri za Kazi Zako kwa Mafanikio Yako

Simulizi
by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Hapa duniani kuna baadhi ya watu wenye makelele na fujo nyingi ambao hujigamba bila hata kuulizwa maswali yanayohusu kazi wazifanyazo.
Aina hii ya watu husahau kuwa kuna nguvu kubwa ya mafanikio pale unapofanya kazi zako kwa ukimya bila fujo wala kujitutumua au kujitangaza. Ni wazi kuwa unapojituma bila kuanika mipango, maendeleo na mafanikio yako hadharani, unaweza kuinua vipaji vingine ndani yako kwani mipango hiyo ni siri na hakuna mwingine unayeshindana naye.
Kwa bahati mbaya siku hizi, kelele zinatuvuta zaidi na majigambo yanatupeleka haraka haraka kiasi kwamba tunafanya matangazo ya mambo yetu bila woga wala kujali madhara yatakayoweza kutokea. Kwa mfano, kijana akianza mahusiano ya kimapenzi, mara anaanza matangazo kuwa ana mchuchu/chuma kipya, hivyo watu wasimwonee wivu. Kwa bahati mbaya mahusiano yakivunjika anaanza kufadhaika na kulalamika huku akisahau kuwa yeye ndiye aliyejiweka hadharani kwanza.
Mfano mwingine, unaweza ukawa unajenga nyumba, kabla hata hujamaliza tayari kila mtu mtaani ana habari. Siyo vizuri, kinidhamu wala kimaadili, hupaswi kuweka bayana mambo yako yote hadharani mapema kiasi hicho. Ni vyema kukaa kimya watu wakaona wenyewe maendeleo yako bila hata kuwashirikisha tokea awali. Acha watu wagundue wenyewe maendeleo yako kimaisha, wakusifie au wakubeze kwani siyo wote watafurahia mafanikio yako.
Hapa tunajifunza kuwa, tuwe na tabia ya kufanya mambo yetu kimya kimya na kwa usiri, hatimaye mafanikio ndiyo yatakayotutangaza.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection