Epuka Marafiki Wanafiki

Caroline Swai - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Kuna aina tofauti za marafiki. Kuna wale wanaojiona kuwa sahihi kwa kila kitu na bora zaidi ya wengine. Watu kama hawa hupenda sana kujisifu na kusifiwa pia. Watu wa aina hii, hata wakikosea hawakubali, bali hutengeneza mazingira ya kukufanya wewe uonekane kuwa ndiye uliyekosea.

Aina hii ya marafiki ni wa hatari sana. Ukitaka kukosana nao jaribu kuwakosoa, hapo ndipo urafiki wenu utakapoisha ghafla.

Kuna wale ambao wanaweza kuja kwako kutaka ushauri, lakini cha ajabu huwa wana majibu yao tayari. Wanachotaka kwako ni kupata ushauri kama wanavyotaka wao, na sivyo utakavyo washauri.

Watu hawa hupenda kukukandamiza kwa kila hali, hata kama wamekusaidia kidogo tu watatangaza kila mahali. Watu wa aina hii huwa hawapendi kuona unaendelea, na huwa hawataki uwazidi kimaendeleo. Hivyo huwa ni watu wa kukukatisha tamaa. Kwa kifupi hawa siyo marafiki wazuri bali ni wanafiki.

Hapa tunajifunza umuhimu wa kuchagua marafiki ambao wana sifa nzuri, wale tunaoweza kusaidiana nao katika hali zote, yaani katika shida na raha.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Kifo Ni Mali Ya Mungu

Next
Next

Lawama Ni Kama Moshi