Kifo Ni Mali Ya Mungu

Simulizi
by Margaret Kayombo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Maisha yetu yana mwisho, hii ni kwa kila mwanadamu. Kutokana na ukweli huo basi, hatuna ujanja wowote wa kukwepa kifo.
Maisha yetu yana ratibiwa na Mungu wetu. Haijalishi umekufa kifo gani lakini siyo lazima pawe na sababu ambayo Mungu ameruhusu kifo kitokee kwako.
Katika jamii zetu kuna matukio mengi ambayo yanawapotosha sana watu. Wengine hudiriki kusema kuwa fulani amekufa, eti kuna fulani mchawi ambaye amemroga na ndiyo maana kafa. Familia nyingi na hata koo nyingi zimeweza kuwa na mifarakano kutokana na mambo ya kufikirika kama haya. Watu wanafikia hatua ya kutozungumza wala kusalimiana.
Hali hii huchangia kudumaza maendeleo kwenye maeneo husika. Pale jamii inapokuwa haina maelewano, hata pakiwa na shughuli za kijamii zihusuzo maendeleo yao, daima patakuwa na mapungufu katika utekelezaji wake.
Kutokana na usemi huu tunajifunza kwamba mwanadamu hana mamlaka ya kukatisha maisha ya mwanadamu mwenzie, ila ni Mungu pekee yake. Vile vile yatupasa tujiepushe na maamuzi ambayo yanaweza kusababisha chuki na fitina ndani ya jamii. Upendo unatakiwa utawale kwenye jamii zetu ili tuweze kuwa na maendeleo.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection