Wanao Subiri Anguko Lako Ni Wengi Kuliko Wanaosubiri Mafanikio Yako

Simulizi
by Margaret Kayombo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Kwenye dunia hii, kila mtu ana njia zake anazozifuata ili afanikishe maisha yake. Hali hii humpata kila mtu, awe baba au mama, lengo ni kuweza kumudu maisha ya hapa duniani. Kutokana na hali hiyo, wengine hufanikiwa kiurahisi na wengine huwa na mapito mengi kabla ya kupata mafanikio.
Katika mchakato mzima wa mafanikio yako utakuta watu wengi sana hawana furaha na mafanikio unayopata. Tena hao huwa ni wengi sana, na huwezi kuamini, wanaweza hata kufanya maombi mabaya ili mafanikio uliyoyapata yatoweke, lengo ni kuwa ufanane nao.
Mara nyingi tumeshuhudia mambo yakitokea hivyo. Ukipata fursa ya kusikia yanayoongelewa juu yako, utagundua kuwa ni maneno ya ajabu sana. Unaweza ukashindwa kuelewa kama hao ni wanadamu au wanyama. Yote haya hutokana na chuki na kukosa upendo kwa binadamu wenzetu. Kuna wachache sana ambao watafurahia mafanikio ya wenzao katika maisha yao.
Kutokana na usemi huu tunajifunza umuhimu wa kuweza kufurahia mafanikio ya wengine. Tukionyesha upendo kwa wenzetu, Mungu atatubariki kwa sababu Mungu wetu ni pendo. Ukionyesha upendo kwa wenzako, Mungu wetu atakuona kuwa wewe, ni mtiifu, na hivyo hataacha kukukirimia, tena vikubwa zaidi ya yule uliyekuwa hufurahii mafanikio yake.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection