Lawama Ni Kama Moshi

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Katika mikusanyiko mingi ya watu, kuna mambo mengi ambayo hutokea. Kuna misuguano ambayo nayo hutokea kati ya mtu na mtu au kikundi na kikundi. Kulaumiana huwa ni kwingi sana kwa sababu kila mtu hujiona ana haki ya kusema chochote alichokuwa nacho, kiwe cha kweli au cha uongo.

Kama moshi ulivyo huwa ukienda juu haurudi tena ndivyo ilivyo kwa lawama. Mtu atakulaumu kwa jinsi akujavyo wewe, lakini sivyo vile ulivyo wewe unavyojijua. Lawama zile haziwezi kukuumiza. Kikubwa ni wewe kujua kuwa yale yamepita na hayatarudi.

Ndio maana ya usemi huu, kama moshi haurudi ukienda umeenda na ndivyo zilivyo kwa lawama, zikienda hazirudi. Usisumbuke na watu wanaokulaumu. Wao ndio kazi yao, hawana jingine la kufanya. Dunia ndivyo ilivyo.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Epuka Marafiki Wanafiki

Next
Next

Mzoea Kutwaa, Kutoa Ni Vita