Mzoea Kutwaa, Kutoa Ni Vita

Grace Mshanga - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Kuna watu ambao wamejijengea tabia ya kupokea tu kutoka kwa wenzao, lakini wao sio wepesi wa kutoa kabisa. Watu wa namna hii, kupokea kwao huwa ni rahisi, lakini inapofika kwa wao kutoa, wanakuwa hawako tayari kabisa kufanya hivyo. Ukweli ni kwamba hata huwa hawakumbuki kurudisha fadhila walizotendewa na wengine.

Kutamani vya kupewa ni tabia ya kibinadamu. Lakini tabia hiyo inakemewa, siyo nzuri. Tusiendekeze tabia hii kwani siyo ya utu hata kidogo. Tujitahidi kuwa tayari kutoa kuliko kuwa tayari kupokea tu. Kama wahenga walivyonena, kutoa ni moyo na sio utajiri. Baraka nyingi zinakuja katika utoaji, na siyo katika upokeaji.

Kwa bahati mbaya, vijana wetu wa leo, wengi wanayo tabia hiyo sana, tabia ya kupenda kupokea tu kuliko kutoa. Kisingizio chao kikubwa ni kuwa hawana kipato. Wanajifanya wajanja. Moyo wa kutoa siyo lazima uwe na kikubwa, la hasha. Chochote mtu alichojaliwa anapaswa kuwa na moyo wa kumumegea aliye mhitaji zaidi.

Wakati mwingine, vijana wetu wanasumbuliwa na uvivu. Vijana wanaaswa kubadilika, waache uvivu, waache roho za kutotosheka, waache roho za umaskini. Wawe na roho za utoaji, waache visingizio.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Lawama Ni Kama Moshi

Next
Next

Akufanyiaye Ubaya.., Mlipe Wema