Akufanyiaye Ubaya.., Mlipe Wema

Grace Mshanga - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Mtu anayekufanyia ubaya ni yule anayekutendea jambo ambalo halikupendezi na ambalo linaweza kukuumiza kwa njia moja au nyingine. Mtu wa namna hii, hutakiwi kumlipa mabaya na wala usiwe na kisasi naye. Ikibidi, mtendee mema na usioneshe kuchukia wala kughadhabika.

Ukimtendea mambo ya kumfurahisha, itakuwa ni fundisho kwake. Kama ni muungwana, anaweza kujisikia vibaya na kuweza kuutambua ubaya aliokufanyia na pengine kuujutia.

Wahenga walisema dawa ya moto ni moto. Mtu anapokufanyia ubaya, nawe ukamlipa wema unampa mtihani mkubwa wa kufikiria nini maana ya jambo ama wema huo. Isitoshe, inaweza ikamfanya aombe hata msamaha kwa kile alichokufanyia.

Watu wengi, hususan kizazi cha sasa, kimejikita kwenye kulipana kisasi pale wanapotendewa mabaya. Tabia hii siyo sahihi kabisa na haina uungwana kabisa.

Usemi huu unatufundisha umuhimu wa kuwa na mahusiano mazuri na jamii inayotuzunguka. Yatupasa tujitahidi kutenda mema ili maisha yawe na maana kwetu sote.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Mzoea Kutwaa, Kutoa Ni Vita

Next
Next

Mwamba Ngoma, Ngozi Huvutia Kwake