Mwamba Ngoma, Ngozi Huvutia Kwake

Simulizi
by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
MASKINI HANA KINYONGO
Umaskini ni ile hali ya kuwa na uhitaji hasa wa yale mahitaji ya muhimu kama vile chakula na mengineyo mengi. Mtu wa aina hiyo huwa hawezi kukataa pale anapoomba, hata kama atakuwa amesemewa mbovu, yeye ataangalia uhitaji wake tu.
Usemi huu unatufundisha kuwa na utu wa kumsaidia mwenye uhitaji.
Siyo vizuri kuwasimanga wenye uhitaji, bali inatupasa tuwasaidie kwa kadri ya uwezo wetu.
Yatupasa tukumbuke kuwa hawa wenye uhitaji hawakuomba kuwa hivyo. Hali kadhalika, na wewe uliye nacho, hukuomba uwe hivyo ulivyo. Tofauti zilizopo baina yako na yule mhitaji ni vigumu kuelezea sababu zake, lakini ni vema tukajua kwamba haya mambo huja kwa zamu. Hata wewe uliye nacho leo, kesho unaweza kujikuta uko katika hali ya umaskini na ikakulazimu kuomba msaada kwa walio nacho.
Sambamba na usemi huu ni ule usemao ‘aliye juu mngoje chini’. Sote tunajua
kuwa hakuna mtu alizaliwa na alicho nacho. Unayemdharau leo huenda akaja kuwa wa msaada kwako kesho. Ikumbukwe kuwa Mungu hakumuumba mtu maskini. Yeye Muumba alitukabidhi dunia na vyote vilivyomo ndani yake.
Kwa hiyo tuwe watu wa kusaidiana katika kuvitumia hivyo vitu tulivyoachiwa bure na Muumba wetu. Kamwe tusiwadharau wenye uhitaji, kesho unaweza ukawa wewe kwani Mtoaji ni Mungu. Kupata ni zamu zamu. Wewe mwenye uhitaji leo, usikate tamaa kwani zamu yako ya kuwa nacho inakuja. Na wewe uliye kuwa nacho, usijisahau sana ukafikiri ndio umefika,? hujui mipango ya yule
mtoaji wetu. Cha msingi, yatupasa tusaidiane katika kila hali. Maisha hayatabiriki. Leo kwako, kesho kwangu.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection