SAMAKI MKUNJE ANGALI MBICHI

Suzan Mwingira
Administrative Assistant
Msemo huu unatufundisha wazazi na walezi kuwalea na kuwafundisha watoto katika maadili na mienendo mizuri ya tabia. Hii huwasaidia wanapokuwa katika mazingira yanayowazunguka waweze kukubalika.
Mtoto anapofundishwa angali bado mdogo inamsaidia kujua jambo zuri na baya kadri anavyoendelea kukua katika maisha yake. Hivyo itamsaidia pindi atakapokuwa mkubwa kukubalika katika jamii na hasa katika maswala mbalimbali ya utendaji kazi. Hivyo wazazi na walezi tujitahidi kuwalea watoto wetu katika misingi iliyo imara. Kwa mfano, adabu, heshima nidhamu, umoja, ukweli, upendo na misingi ya kidini.