Jifunze Leo Kwa Ajili Ya Maisha Ya Kesho

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Maisha yako ya kesho yanategemea sana na yale unayoyafanya leo. Maisha unayoyaishi leo ndio dira yako ya kesho. Kwa kawaida, watu wengi huwa tunajisahau sana tunapokuwa tumepata. Mara nyingi huwa tunakosa fikra ya kujua kuwa hapa duniani, mambo yanaweza kubadilika saa na wakati wowote. Imekuwa ni tabia ya baadhi ya watu kubadilika kitabia pale wanapopanda vyeo kazini ama maisha yao yanapobadilika kwa kuwa na kipato zaidi. Inapokuwa hivi, karibu kila kitu kitabadilika, pamoja na jinsi wanavyotembea, wanavyoongea na hata lugha wanayotumia, nayo pia hubadilika. Mabadiliko hayo hayaishii tu hapo, hata marafiki watakaokuwa nao pia hubadilisha.

Ikifikia hatua hiyo, tunaweza kusema kuwa watu hawa wanakuwa wameshindwa kuijua kesho yao itakuwaje. Wanakuwa hawajui nani atakuwa ni wa msaada kwao. Yatupasa tuitengeneze leo ili kesho yetu iwe njema. Yatupasa tumjali kila mtu kwa hali na uwezo wowote walio nao. Tunatakiwa tuyafanye haya kwa sababu hatujui mwisho wetu utakuwaje kwani hata na sisi hali zetu zinaweza kubadilika wakati wowote, dunia yetu ndivyo ilivyo, ni kigeugeu. 

Kutokana na yote hayo, hapa duniani, yatupasa tumheshimu kila mtu, awe mkubwa ama mdogo. Kila mtu angependa kuishi maisha mazuri, maisha yanayoeleweka, maisha yenye mwelekeo. Lakini kutokana na sababu ambazo mara nyingi huwa ni nje ya uwezo wetu, hali ya maisha huwa inabadilika na kuwa vile, ila ni nyakati na majira tu ndio inakuwa tofauti. Sawasawa na maandiko matakatifu yasemavyo kuwa majaribu ni mtaji kila mtu hana budi kuyapitia.Tengeneza siku yako leo kwa ajili ya maisha ya kesho.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community - eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO's mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania

Previous
Previous

Tuache Kulea Watoto Kama Mayai

Next
Next

Kikulacho Ki Nguoni Mwako