Usisahau Mwanzo Wako

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Kwenye maisha huwa kuna mahala pa kuanzia. Mara nyingi huwezi kuanza na kila kitu ambacho unaona ndio uhitaji wako. Mathalani, utaanza kwa kulala chini kwa sababu kitanda hauna. Utajibidisha kwa kila hali mpaka siku moja upate kitanda. Hali kadhalika, vyombo vya jikoni navyo utakuwa huna. Waweza kuanza na sufuria moja, ugali na mboga hiyo hiyo. Lakini pole pole utatafuta vyombo vingine na hatimaye utakuja jikuta mambo na mazuri. Pole pole ndio mwendo, na pia subira huvuta kheri, waswahili husema.

Palikuwa na dada mmoja ambaye alianza maisha akiwa hohe hae. Kwa bahati nzuri alimpata mshikaji ambaye alikuwa na unafuu wa maisha. Lakini ni dhahiri pia huyu aliyempata, naye alipata baada ya kusota na kuhangaika kwa muda mrefu. Huyu dada aliona kama kafika, basi alizisahau shida zake zote na kuona kuwa maisha ni safi na kwamba hakuna tena shida hapa duniani. 

Kama ilivyo ada ya mwanadamu, safari yetu ni fupi sana hapa duniani. Huyu dada hakupata bahati ya hakuishi na huyu bwana kwa muda mrefu. Bwana huyu alikutwa na umauti, akafariki. Kifo cha huyu bwana ndio ulikuwa mwanzo wa matatizo ya huyu dada. Binti kwa hakika, alichanganyikiwa, maisha yalirudi kuwa mabaya kuzidi pale mwanzo na kwa kweli, alipata msongo wa mawazo, akawa anaongea peke yake.  

Wakati alipokuwa anajiona huwa amepata, alikuwa anawadharau wale ambao aliwaona kuwa walikuwa hawana chochote. Hivyo basi, sasa ilikuwa ni zamu ya wao pia kuanza kumdharau na kumcheka. Kwa hakika, ikawa usemi wa kutesa kwa zamu unafanya kazi kwenye hali hiyo.

Cha msingi katika maisha yetu ya hapa duniani, yatupasa tuishi kwa kuheshimiana. Ukiona umepata leo, kumbuka ulikotoka kwani unaweza ukakikuta na hali yoyote, wakati wowote. Tukumbuke pia, kila mtu ana mwanzo tofauti na mwingine. Dada katika simulizi hii alipobahatika kukutana na mtu mwenye nacho alijisahau kabisa alikotoka. Aliwadharau wenzie na kuwaona kuwa ni wa chini na kwamba hawafai kuchangamana naye. Leo anaporudia hali yake ya zamani anakosa mahali pa kukimbilia kwani alijitoa kwenye kundi hilo la walala hoi.  

Kuna mengi ya kujifunza kutoka simulizi hii. Tunaaswa kutoudharau mwanzo wetu, kwa sababu kila jambo lina mwanzo na mwisho wake. Kuwa makini katika maisha yetu iwe ndio msingi bora wa kuishi hapa duniani. Wahenga walinena, dunia ni tambara bovu, haitabiriki, leo iko hivi, kesho itakuwa vile, na maisha ndivyo yalivyo, hayatabiriki kamwe.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Akumulikaye Mchana, Usiku Atakuchoma

Next
Next

Dhuluma Haidumu