Akumulikaye Mchana, Usiku Atakuchoma

Tap Elderly Women's Wisdom for Youth (TEWWY)

Simulizi

by Tap Elderly Women's Wisdom for Youth (TEWWY).

Mchana ni wakati ambapo vitu vyote vinaonekana waziwazi bila ya taabu yoyote. Usiku ni wakati wa giza, ambapo ni taabu kuona kitu au vitu waziwazi. Kwa hiyo basi, ikiwa mtu hakuweza kukuona vizuri wakati wa mchana, hata ikamlazimu awashe taa akumulike ili akuone, hiyo ni ishara ama dalili tosha kuwa macho ya mtu huyo yana walakini ama matatizo.

Usemi huu unatufundisha kuchukua tahadhari ama kujihadhari na watu waovu ambao waliwahi kutufanyia ubaya au fitina, tukanusurika. Kwa kuwa watakuwa wametukosa kwa hilo kwa wakati ule, wanaweza wakatutafutia jingine la kutuangamiza. Ndiyo maana inasemekana kuwa ikiwa walitumia taa mchana kweupee, wakati jua linawaka kutumulika, je ikifika usiku si ndio watatuchoma kabisa? 

Yatupasa tutafakari, yatupasa tujihadhari.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Chiriku Na Panzi

Next
Next

Usisahau Mwanzo Wako