Binadamu Ana Nyuso Mbili, Kaa Nae Kwa Akili

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Mara nyingi tumeona kuwa siyo watu wote wanaokuzunguka ni wema kwako. Wewe unaweza ukajiona kuwa ni mwema kwa watu na wao , vivyo hivyo, ukawaona ni wema kwako. Katika imani hiyo unaweza ukajiridhisha na kuona kuwa una ndugu au marafiki wa haja, marafiki wa kukimbiliwa ukiwa na shida.

Aghalabu, utakuja kushangaa siku utakapopata shida. Yule ambaye ulimfikiria kuwa atakuwa ndio bega lako la kuegemea wakati wa shida zako, hatakuwa tayari kutoa msaada wowote katika shida yako. Badala yake, yeye ndiye atakayekuwa kinara wa kwanza wa kuitangaza shida yalo kwa watu wengine. Atawaeleza mambo ya uongo na pia ya kukatisha tamaa juu yako. Atawaeleza siri zako zote ulizokuwa umemumegea katika kipindi cha uswahiba wenu. 

Kutokana na mlivyokuwa karibu, watu wakisikia hayo yanasemwa dhidi yako, lazima wataamini maneno yake. Hawatategemea rafiki mpenzi kama yule akusemee mambo ya uongo mbele za watu. Wakisikia habari zako za ndani, wale ambao ulikuwa ukiwaona kuwa si wema kwako, nao wataongezea kusema mabaya zaidi juu yako, ili mradi tu na wao waweze kutimiza azma yao. Pengine nao walikuwa wanatafuta nafasi ya kukuchafua lakini walikuwa bado hawajaipata, sasa watakuwa wamepata nafasi murua ya kukumaliza. Kwa ujumla, nao watachangia kwa kukuchafua vibaya zaidi. Lakini, ikumbukwe kuwa chimbuko la yote hayo ni yule ama wale maswahiba wako, uliokuwa ukiwaamini na kuwathamini, mliokuwa mmeshibana kupita maelezo. 

Usemi huu unadhihirishwa na kuungwa mkono na ule usemi wa “Cheka nao, lakini sio wema kwako”. Wahenga walinena, ni aheri ukutane na mnyama mkali kuliko ngulu mbili. Ngulu mbili ni binadamu asiye kuwa na fadhila. Na wengine huongezea kusema, ni heri umfadhili punda, binadamu hutamuweza. 

Tunaaswa kuwa makini katika mahusiano yetu na binadamu. Mwanadamu hatabiriki, anaweza kuwa mbaya kuliko unavyomdhania. Anaweza kubadilika wakati wowote. Cha msingi, tuwe makini.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Elimu Bila Vitendo Ni Sawa Na Bure

Next
Next

Kisa Cha Kuku Na Kanga