Upendeleo Au Ubaguzi Ndani Ya Familia Siyo Mzuri

Caroline Swai - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu, hivyo tunapaswa kushukuru. Mungu anapokupa watoto wawe wa kiume, kike au mchanganyiko inabidi uridhike na kumshukuru Mungu, kwani kuna wengine ambao hawakujaliwa kupata kabisa.

Kuna wazazi ambao wana upendeleo au ubaguzi wa waziwazi kwa baadhi ya watoto wao wenyewe. Jambo hili siyo sawa.

Kama mzazi, hupaswi kuonyesha ubaguzi au upendeleo wa aina yoyote kwa watoto wako, kwani kwa kufanya hivyo utakuwa unawatengenezea watoto wako chuki, mtafaruku na kutoelewana. Upendeleo huu unaweza ukawatengenezea mazingira hasi katika maisha yao ya baadaye.

Wazazi tunaaswa kuwapenda watoto wetu wote bila upendeleo au ubaguzi, kwani kwa kufanya hivyo kutaepusha kutengeneza bomu la baadaye kwa watoto wetu.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Mbuzi Hula Kadiri Ya Urefu Wa Kamba Yake

Next
Next

Utaula Wa Chuya Kwa Uvivu Wa Kuchagua