Mbuzi Hula Kadiri Ya Urefu Wa Kamba Yake

Avelina Hokororo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Avelina Hokororo (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Mbuzi ni mnyama anayefugwa kama wanyama wengine. Akipelekwa machungani huwa anafungwa kamba mguuni ili kumuwekea mipaka ya malisho yake. Mara nyingi akiachiwa huru au akikata kamba anaenda kufanya uharibifu kwa kula kwenye mashamba ya watu na mwenye mbuzi hupata kesi kubwa. Mara nyingine huweza hata kulipishwa kwa uharibifu huo uliosababishwa na mbuzi wake. Hii ndio sababu kuu ya kufungwa kwa kamba. 

Usemi wangu huu wa leo ni fundisho kwa wanandoa. Unapofunga ndoa, iwe ya kanisani, ya msikitini au ya serikalini, ni sawa na kufungwa kamba mguuni. Unatakiwa kuwa mwaminifu kwa mwenza wako. 

Lakini utakuta mume au mke anakosa uaminifu na kutoka nje ya ndoa. Inapotokea hivyo basi mhusika anakuwa amekata kamba. Anaanza kushambulia vibinti vingine vidogo, matokeo yake yanakuwa ni aibu tupu. 

Hali kadhalika, kwa akina mama ambao wanakata kamba na kujiingiza kwenye mahusiano na vijana ambao wengine wanakuwa sawa sawa na umri wa watoto wao, nao wanakuwa wamefanya unyama usiovumilika.

Mwisho wa matendo yote haya, ya mume ama mke kukata kamba huwa ni fedheha kubwa. Mara nyingi ndoa za aina hii, huwa na migongano kila uchao, pamoja na kusambaratika iwapo wazee hawataingilia kati kuwashauri, yaani kuwafunga kamba tena. 

Katika ndoa, mara nyingi sana kinachofanya ndoa kuyumba ni kukosa uaminifu kwa mwanandoa mmoja kwa mwenzake, awe baba au mama. Hapo utasikia mtu kajiua kwa sababu ya wivu wa kimapenzi. Ukweli huwa mmojawao hakuwa mwaminifu kwa mwenzie, kikubwa atakuwa alikata kamba.  

Wana ndoa, mnashauriwa kutokata kamba zile ambazo mlifungwa nazo. Yawapasa mle kwenye eneo lenu mliloruhusiwa siku ya ndoa yenu. Kwa kufanya hivyo, nyumba zenu zitakuwa na amani tele. Hata msongo wa mawazo mtausikia tu kwenye vyombo vya habari. Hautakuwepo. Pia hata vifo vya kujiua vitapungua kama si kumalizika kabisa. Zingatieni hayo, kuleni urefu wa kamba zenu, acheni ulafi.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection 

Previous
Previous

Shida Haipigi Hodi

Next
Next

Upendeleo Au Ubaguzi Ndani Ya Familia Siyo Mzuri