Shida Haipigi Hodi

Simulizi
by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Shida ni tatizo au changamoto inayomfika mwanadamu. Hodi ni neno linalotumika badala ya swali la: “naweza kuingia?" Hapa anaposema shida haina hodi sio kweli maana mwanadamu anapopatwa na tatizo ataingia kwa jirani na kutoa shida zake ikibidi kuomba msaada ili atatue changamoto zake. Shida inaweza kukupeleka hata mahali ambapo hujawahi kufika.
Usemi huu unatukumbusha kuishi vizuri na jamii inayotuzunguka. Kuna usemi usemao, “halahala jirani” ikiwa na maana kuwa, hata kama umepata shida, jirani yako ndio wa kwanza kufika kwako na kukusaidia.
Alikuwepo baba mmoja ambaye alikuwa hahudhurii kwenye matatizo na shughuli za majirani zake. Mama yake alipokuwa akiumwa, alikuja kuugulia nyumbani kwake. Kwa bahati mbaya, umauti ulimkuta hapo kwa mtoto wake. Tofauti na matarajio yake, majirani hawakujitokeza. Alijikuta yuko yeye peke yake na mke wake.
Majirani wengi walimdhihaki na kusema akae na hela zake. Hali hii ilimlazimu ajishushe. Alilazimika kuomba radhi kwa jirani zake. Tokea siku hiyo alipata funzo. Kila shida ama tatizo likitokea mtaani kwake, yeye ndiye anakuwa wa kwanza kufika.
Hapa tunajifunza mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuwa na utu tunapoishi hapa duniani. Yatupasa tuzingatie kuwa sisi binadamu tunategemeana hivyo kusaidiana na kutiana moyo ni wajibu wa kila mtu. Fundisho ni kwamba uwezo wa mtu hautakiwi kumtenganisha na jamii inayomzunguka. Hakuna aliyekamilika hapa duniani. Shida inagonga mlango kila nyumba. Binadamu tunahitajiana. Hatuna ujanja. Tujifunze kushirikiana.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection