Ulimi Ulimponza Kichwa

Simulizi
by Avelina Hokororo (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).
Ulimi ni kiungo kidogo ndani ya mwili, hukaa mdomoni na kumwezesha mtu kuongea vizuri. Kama ulimi haufanyi kazi basi mtu hawezi kuongea vizuri na mara nyingi huwa bubu.
Kuna siku, mtu mmoja alikuwa anagombana na rafiki yake. Katika kurushiana maneno mbalimbali ya maudhi mbele za watu, wakataka kupigana. Lakini watu wakaawamulia na kuwasihii wasipigane. Hali kadhalika, waliwasihii wasameheane.
Basi yule rafiki yake aliamua kuondoka mahali pale. Kabla hajaondoka, mgomvi wake akamwambia, “Tutaona kama kesho utaamka ukiwa hai”. Rafiki yake akaondoka, yeye akaingia ndani kwake akalala.
Siku moja usiku, akiwa anaelekea nyumbani kwake, njiani akavamiwa na majambazi. Walimpiga hadi akapoteza uhai. Ilipofika asubuhi, habari zilienea kuwa yule rafiki yake ameuawa. Mshukiwa wa kwanza alikuwa yule mtu aliyesema kesho hataamka akiwa hai.
Wakaja Polisi pale nyumbani kwake wakamkamata. Alilia sana. Mashahidi waliokuwepo walithibitisha kuwa, kweli alisema, lakini baada ya hapo hawakumuona tena kutoka ndani mwake mpaka ile asubuhi anapokamatwa. Lakini kutokana na maneno aliyokuwa ameyatamka, ulimi wake umemponza. Umemfanya atuhumiwe yeye na akashitakiwa kwa kesi ya mauaji.
Usemi huu unatufundisha tuwe waangalifu sana kwa maneno tunayotamka. Kwa mfano, hata tunapoongea na watoto wetu tusiwanene maneno ya laana. Maneno kama vile, ‘utaona mwenyewe mbele ya safari ya maisha yako’ na mengine mengi. Na kweli mtoto anaweza kupata mabalaa ya kukosa kazi, kukosa mke mwema au kuwa mlevi kupindukia wa vilevi vyote. Wewe mwenyewe utaanza kumlilia Mungu anakuonea. Wakati huo unakuwa umesahau kama ulikuwa unamnenea mara kwa mara maneno mabaya, maneno ya laana pale alipokuudhi.
Mzazi, hata kama mtoto anakuudhi kiasi gani, yakupasa umtamkie maneno yanayofaa ya kumuonya tu na hata kumtia moyo ili asije akakutana na mabalaa mbele ya safari. Maneno ya mzazi yana uzito mkubwa kwa mtoto. Tuepuke kuwatamkia maneno ya kuwapa mikosi ama mabalaa katika maisha yao. Mwisho wa siku yakimkuta mambo mabaya, hata wewe mzazi utaumia na kubaki unahangaika sana.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection