Wagombanapo Ndugu, Chukua Jembe Kalime, Wakipatana, Chukua Kapu Kavune

Simulizi
by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Ndugu ni watu waliozaliwa katika familia moja au ukoo mmoja. Ugomvi ni hali ambayo hujitokeza kwa kutokuelewana mtu na mtu. Ugomvi huu unaweza ukafikia hata kupigana.
Jembe ni nyenzo au kifaa kinachotumika kulimia, wengi huita jembe la mkono. Kikapu kinatumika kuweka mazao au mavuno ya aina yoyote, kama mahindi, nyanya, na kadhalika.
Msemo huu unamaanisha kuwa ndugu wanapogombana wewe nenda ukazalishe na watakapopatana nenda ukavune. Kwa maneno mengine, tunafundishwa kuwa tusiingilie ugomvi wa ndugu kwa sababu damu ni nzito kuliko maji. Watakapopatana wewe ndio utakuwa mbaya na utaonekana kuwa ni mchonganishi. Na ugomvi ukihamia kwako hautaisha. Hali kadhalika, watakapopatana wala hawatakuhusisha.
Yakupasa wewe uwe msuluhishi tu, na sio mchonganishi au muingilia mambo ya ndugu. Mambo ya ndugu, yaache yamalizwe na ndugu wenyewe, usiyaingilie kamwe, yasije yakakushinda bure.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection