Unachokifanya Leo Kinatengeneza Kesho Yako

Simulizi
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Jambo lolote ambalo mwanadamu analifanya linategemea sana maandalizi aliyojiwekea kwenye mipango na mikakati yake. Mafanikio hayawezi kuja kwa kufikiria tu, bali ni kwa utekelezaji wa yale uliyojipangia.
Hii ina maana kuwa huwezi ukaamuka asubuhi na kuanza kufanya jambo ambalo hukulipanga kufanya siku hiyo. Unapotoka nje ya mipango yako usitegemee kufanikisha jambo lolote. Kila jambo linatakiwa kuwa na maandalizi yake. Kumbuka, unachokifanya leo ndicho kitakacho kuongoza kesho yako. Mafanikio hayaji kiurahisi rahisi tu. Lazima uwe mtu wa mipango na mikakati.
Hata hivyo, siyo rahisi kutekeleza mambo yote kwa wakati mmoja. Inakupasa uzingatie na uangalie umuhimu wa jambo hilo kwa wakati huo.
Msemo huu unatufundisha kuwa makini na maisha yetu ya kila siku. Tuishi kwa kuangalia na kuzingatia vipaumbele tunavyojiwekea. Hali kadhalika, inatupasa tuviheshimu vipengele hivyo, ama siyo vitakuwa havina tija.
Kumbuka, maisha bila mipango huwa na mwisho usioeleweka. Tengeneza mipango inayotekelezeka na ambayo itakuwezesha kufikia mafanikio unayoyatarajia.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection