Mkuki Kwa Nguruwe, Kwa Binadamu Mchungu

Grace Mshanga - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Mkuki ni silaha ya jadi inayotumika kuwinda wanyama wakubwa. Hapa kwenye msemo huu ina maana kuwa maneno makali ya kuumiza, kudhuru na kubomoa, kwetu sisi wanadamu inaonekana kuwa, ukimtamkia mtu mwingine unaweza kuona ni kawaida na sawa. Lakini maneno hayo hayo ukitamkiwa wewe utaona kuwa ni mabaya na utachukia kupindukia.

Hivyo tukiwa katika dunia hii yatupasa tutafakari na kuhchagua maneno ya kumtamkia mwenzio. Jiulize kwanza, ‘Je nikimtamkia maneno haya, yatakuwa na madhara au faida gani kwake? Je, yatambariki? Atayfurahia? Yatamtia moyo na kumfanya asonge melee’? Ukipata majibu ya haya maswali ndipo unaweza kuyatumia maneno uliyodhamiria kumwambia ama kutomwambia.

Epuka kumwambia mtu maneno ya kumdidimiza au kumkatisha tamaa. Unachopenda kutendewa wewe, jitahidi sana umtendee na mwenzio pia. Sote ni binadamu, tukwepe kutoa maneno ambayo tusingependa kuambiwa sisi na wenzetu. Maneno ya kuumiza tusiyatumie kwa wenzetu.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Kuku Mgeni Hakosi Kamba Mguuni

Next
Next

Kikulacho Ki Nguoni Mwako