Kuku Mgeni Hakosi Kamba Mguuni

Simulizi
by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Kuku ni ndege afugwaye kwenye makazi ya wanadamu. Kuku huchukuliwa kuwa ni kitoweo cha heshima kwa wageni wa hapo majumbani kwa watu.
Tunaposema kuku mgeni hakosi kamba mguuni, tunamaanisha kuwa kuku huyo, yupo mahali ambapo hajapazoea. Lengo la kumfunga kamba mguuni ni kumwezesha kutambulika kiurahisi, asije akapotea. Akishazoea, kamba hutolewa na kuku huachwa huru.
Hapa tunajifunza kuwa tuendapo mahali ugenini tunatakiwa kujifunza mazingira ya hapo mahali kwanza. Kuwasikiliza wenyeji ili kujua nini hawapendi na nini wanakipenda, hilo ndio huwa jambo la msingi. Hii ni kwa sababu kila mahali pana taratibu zake za maisha. Kuna msemo pia usemao, ‘Ukiwa Roma, fanya kama Warumi wanavyofanya’. Hutakiwi kupeleka ujuaji wako sehemu ambayo huifahamu na pia hujaizoea.
Tunaonywa kutojifanya wajuaji tukienda ugenini. Yatupasa tutulizane kwanza. Huo ndio uungwana ambao kila mwanadamu anatakiwa aufuate. Epuka kujifanya unajua kila kitu. Kumbuka, hakuna mwanadamu ajuaye kila kitu. Ukiwa ugenini, angalia kwanza kwa lengo la kuyajua mazingira, chunguza kwanza na tafakari hatua za kuchukua. Ukiwa ugenini, una sababu ya kujifunza kila kitu
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection