Bora Mchawi Kuliko Mfitini

Simulizi
by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Dunia imejaa fitina za kila aina. Wako watu ambao kazi yao kubwa ni kufitinisha au kuchonganisha watu. Mara nyingi, hali hii hutokana hasa pale wanapoona fulani anaelewana vizuri na fulani. Watatafuta kila njia ili wawakosanishe.
Sambamba na hilo, kuna watu ambao hujulikana kuwa ni mafundi au wataalamu. Inasemekana kuwa mafundi hao hutumia nguvu za giza ili kuwavuruga watu ama kuwakosesha amani.
Makundi haya yote mawili yanaenda sambamba kwani yote mawili huvuruga amani za watu. Hapa ndio unakuta watu wengi wakisema “ Aheri ya mchawi kuliko mfitini”. Pengine hii inaweza kuwa ni kutokana na sababu ya kwamba mchawi huwa haonekani kwa macho, tofauti na mfitini.
Usemi huu unatufundisha kuwaepuka wafitini katika jamii zetu. Wafitini wako wengi na ni kila mahali. Tusipokuwa waangalifu tunaweza kujikuta mahali pabaya. Tunaweza kujikuta tumekosana na watu wengi bila sababu ya msingi. Hii ni kutokana na sumu iliyomwagwa na wafitini ambao wanakuwa wamekutengenezea uadui. Binadamu kiumbe mzito kweli kweli. Yatupasa kuchukua tahadhari, siyo kuamini kila unachoambiwa na mtu kuhusu mtu mwingine.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection