Akiba Haiozi

Grace Mshanga - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

SIFA ZA NDEGE NI MANYOYA

GRACE MSHANGA

Ndege ni viumbe hai na wana mabawa na wana miguu miwili. Wana uwezo wa kuruka. Chakula chao ni wadudu na nafaka.

Ndege wengi wanaliwa na binadamu na huwa ni kitoweo kizuri kwa ajili ya wanadamu. Kuna ndege wengine kama kunguru na tai ambao tunahisi kuwa hawaliwi na watu hapa nchini .

Sifa ya ndege ni manyoya yao. Ndege wengi hutambuliwa kwa manyoa yao. Ukiweka mafungu ya manyoya, waweza kujua kuwa fungu hili la manyoya ni la kanga. Hali kadhalika unaweza kujua kuwa fungu lile kule ni la tausi na lile pale ni la njiwa, na hilo hapo ni la kunguru. Hii ina maana kuwa manyoya yanatuwezesha kujua na kutambua aina ya kila ndege. Muumba wetu ametutofautishia aina ya ndege aliotuwekea hapa duniani kwa kuwapa manyoya tofauti.

Hata sisi wanadamu tunatambuliwa kwa sifa zetu tulizo nazo. Unaweza kuambiwa sifa za binadamu chungu nzima. Mathalani, unaweza ukamjua mtu kwa uchoyo wake, uongo, umbea, uchonganishi na hata uzushi wake. Hali kadhalika, kuna watu wenye tabia au sifa ya kujisikia sana. Wengine wana tabia ya kudhulumu wenzao. Kuna wale ambao wana roho mbaya ama wana kinyongo na wenzao.

Ni mara chache utasikia kuhusu watu wema, wenye upendo. Wako wale wenye moyo wa kusaidia majirani zao. Hao hutambulika sana kwenye maeneo wanayoishi.

Sifa hizo mbaya zilizotajwa za binadamu ni zile ambazo husikika mara kwa mara. Yatupasa kama binadamu tuziepuke sana sifa hizo mbaya ili tuweze kuishi vizuri na watu. Tunatakiwa tuwe na sifa zilizo nzuri za kuibariki jamii inayotuzunguka na ndiyo itatuletea kuishi maisha marefu. Tutofautishwe utu wetu kama vile ndege tunavyoweza kuwatofautisha na ndege wengine kutokana na manyoya yao.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Avuae Nguo Huchutama.

Next
Next

Tone La Maarifa.